Sasha Obama alikuwa wapi wakati ya hotuba ya mwisho ya babake?

Mwana mkubwa wa Obama Sasha, mkewe Michelle Obama na rais Barrack Obama wakati wa hotuba yake ya mwisho
Image caption Mwana mkubwa wa Obama Sasha, mkewe Michelle Obama na rais Barrack Obama wakati wa hotuba yake ya mwisho

Huku raia wa Marekani wakitizama hotuba ya mwisho ya rais Obama mjini Chicago siku ya Jumanne usiku, wengine waliwachwa na swala moja.

Sasha Obama alikuwa wapi?. Picha ya kwaheri iliopigwa ilimuonyesha Obama ,mkewe na mwanawe mkubwa Malia mbele ya jukwaa, lakini msichana hyo wa miaka 15 hakuonekana.

Imeelezewa kwamba msichana huyo alikuwa akifanya mtihani katika shule ya Sidwell mapema siku ya Jumatano.

Shule hiyo ndio imewafunza wana wa marais kwa miaka mingi akiwemo Chelsea Clinton.

Haki miliki ya picha Twitter
Image caption Ujumbe wa Twitter uliotumwa na baadhi ya raia nchini Marekani wakitaka kujua Sasha aliko

Kwa hivyo imekuwa ikitumika kukabiliana na wanafunzi ambao wamekuwa wakikosa darasa kutokana na kuhudhuria maswala ya uongozi.

Lakini hilo halikusitisha kuanzishwa kwa #WhereIsSasha katika mitandao ya kijamii.

Baadhi ya watu walitarajia kwamba anajaribu kumzuia Donald Trump kuingia ikulu ya Whitehouse.