Alipa kodi kwa kutumia toroli 5 za sarafu

Nick Stafford alikodisha toroli tano kusafirisha malipo ya kodi yake. Haki miliki ya picha DAVID CRIGGER/BHC
Image caption Nick Stafford alikodisha toroli tano kusafirisha malipo ya kodi yake.

Mfanyibiashara mmoja nchini Marekani ambaye amezozana na idara ya magari nchini humo DMV amelipa kodi yake ya dola 3,000 kwa kutumia mikokoteni mitano iliojaa sarafu 300,000

Nick Stafford kutoka Cedar Buff, Virginia, aliwasilisha sarafu nyingi hatua iliolazimu mashine ya kuhesabu sarafu hiyo ya Idara hiyo kushindwa kuzihesabu.

Hatua hiyo inajiri kufuatia mgogoro kati yake kuhusu kuwasiliana na wafanyikazi kuwauliza kuhusu kodi yao.

Iliwalazimu wafanyikazi kutumia saa saba wakihesabu sarafu hizo hadi usiku. Walimaliza kazi hiyo ya kuhesabu mapema siku ya Alhamisi.

Haki miliki ya picha DAVID CRIGGER/BHC
Image caption Bwana Salford alikuwa na sarafu 300,000

Bwana Stafford aliambia BBC aliwasilisha pingamizi yake kwa sababu alizitaka idara za serikali kuangazia na kutoa majibu kwa maswala yanayowakumba raia.

"Haijalishi iwapo utalipa dola 300 kwa mwaka kama kodi au dola 3000 kwa mwaka kama mimi kwa sababu uti wa mgongo wa taifa lililo na demokraisa huru ni sharti liwe na serikali ilio na uwazi, alisema.

Bwana Stafford ameelezea katika mtnadao wake kwamba mgogoro wake na DMV ulizuka kwa sababu idara hiyo haikutaka kumpatia nambari za simu za moja kwa moja kuhusu afisa wa kuwasiliana naye ili kusajili magari matatu na kulipa ushuru kwa kuwa anamiliki nyumba tatu katika maeneo 3 tofauti.

Aliwasilisha ombi la kutaka kupewa nambari ya moja kwa moja kulingana na Bristol Herald Courier na akapewa nambari ya simu ambayo angepiga.

Lakini alipoitumia aliambiwa kwamba haingeweza kuitumia kuuliza maswali.

Bwana Stafford alitaka kujua nambari hizo za moja kwa moja za maafisa wengine tisa ijapokuwa Idara hiyo tayari ilikuwa imemshughulikia swala lake.

Na ombi lake lilipokataliwa alienda mahakamani kuwasilisha malalamishi yake.

Mapema wiki hii jaji mmoja alipinga maombi yake matatu aliowasilisha ,akikataa maombi alilowasilisha kwa DMV na wafanyikazi wake wapigwe faini.

Hatahivyo wafanyikazi wa idara ya magari baadaye walimpatia nambari hizo alizotaka na tayari amezichapisha katika mtandao wake.

Bwana Stafford anasema kuwa idara ya magari ililazimika kukubali malipo yake kwa sababu sheria ya Marekani kuhusu sarafu mwaka 1965 inasema sarafu ni fedha halali na zinaweza kutumika kulipa madeni, kodi na mishahara

Haki miliki ya picha DAVID CRIGGER/BHC
Image caption Idara ya ushru nchini Marekani ilitumia wakati mwingi kuhesabu fedha hizo