Harakati za kuondoa ObamaCare zaanza Marekani

Wabunge wa Republican waanzisha harakati za kuondoa bima ya Afya ya Obamacare iliozinduliwa na rais Obama
Image caption Wabunge wa Republican waanzisha harakati za kuondoa bima ya Afya ya Obamacare iliozinduliwa na rais Obama

Wabunge wa Congress nchini Marekani, ambao wengi wanawakilisha chama cha Republican, wamepiga kura ya kuanza kubadilisha sheria ya Bima ya afya inayofahamika kama Obama care iliozinduliwa na rais Barrack Obama

Bunge la seneti pia limepitisha kura hiyo, ambayo inahitaji kamati za bunge kuanza kuandika upya sheria hiyo.

Hata hivyo baadhi ya wabunge wameonekana kupinga kura hiyo, wakisema ni lazima kuwe na sheria mbadala, kabla ya kufuta ObamaCare.

Hata hivyo bwana Trump anayetarajiwa kuchukua hatamu za uongozi wiki ijayo, amesifu wabunge hao, na akaandika kwenye Twitter, 'ObamaCare itazikwa kwenye kaburi la sahau hivi karibuni.