Mtoto aliyeibwa apatikana hai miaka 18 baadaye

Mtoto aliyeibwa Kamiyah Mobley kushoto na mwanamke aliyepatikana naye Gloria Williams Kulia Haki miliki ya picha JACKSONVILLE SHERIFF'S OFFICE
Image caption Mtoto aliyeibwa Kamiyah Mobley kushoto na mwanamke aliyepatikana naye Gloria Williams Kulia

Mtoto mchanga aliyeibwa katika hospitali moja ya jimbo la Florida nchini Marekani, amepatikana akiwa hai baada ya miaka 18 katika jimbo la South Carolina.

Kamiyah Mobley ,aliibwa kutoka kwa mamake akiwa na umri wa saa 8 pekee.

Mwanamke aliyejifanya kuwa muuguzi alisema mtoto huyo alikuwa mgonjwa na angehitaji uchunguzi wa kimatibabu.

Baadaye alitoweka na mtoto huyo.

Mwanamke anayeishi na mtoto huyo, Gloria Williams, ametiwa mbaroni baada ya polisi kupashwa ripoti.

Familia halisi ya mtoto huyo ilijuzwa taarifa kuhusu kupatikana kwake, baada ya uchunguzi wa vinasaba kubaini utambulisho wake.