Kijana wa familia masikini apelekwa shule kwa helikopta Kenya

Kijana Kelvin akiwa katika ndege iliotumika kumsafirisha hadi shule ya upili aliyojiunga nayo

Chanzo cha picha, THE SAMARITANS

Maelezo ya picha,

Kijana Kelvin akiwa katika ndege iliotumika kumsafirisha hadi shule ya upili aliyojiunga nayo

Mtoto mmoja kutoka jamii masikini nchini Kenya amesafirishwa hadi shule mpya ya upili anayojiunga nayo kwa helikopta baada ya muungano mmoja wa wanajeshi wa zamani wa angani kusema kuwa utamlipia karo ya shule.

Kelvin Muriuki alikuwa bora katika shule yake katika mtihani wa mwisho wa shule za msingi , lakini umasikini ukamlazimu kufanya kazi katika timbo, familia yake imesema.

Muungano huo wa maafisa wa zamani wa jeshi la angani ulijitolea kumlipia karo na kumsafirisha kwa ndege hadi katika shule yake mpya.

Sasa ndoto ya Kelvin imefufuka na anataka kuwa rubani.

Watoto wengi huwacha shule nchini Kenya kutokana na ufukara.

Muungano huo umesema kuwa utamlipia karo Kelvin za dola 530 kila mwaka hadi atakapomaliza shule ya upili 2020.

Aliwasili katika shule yake mpya mjini Karicheni huko mkoa wa kati baada ya kupewa usafiri wa ndege hiyo iliochukua dakika 20 kutoka shule anayotoka, kulingana na ripota wa BBC Abdinoor Aden katika mji mkuu wa Nairobi.