Kiongozi wa Palestina akutana na Papa Francis

Rais wa Palestina Mahmoud Abbas akutana na papa Francis mjini Vatican Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Rais wa Palestina Mahmoud Abbas akutana na papa Francis mjini Vatican

Rais wa Palestina, Mahmoud Abbas, anakutana na kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis huko Vatican, kabla ya kufungua ubalozi wa Palestina huko.

Ubalozi huo unafunguliwa miaka minne baada ya Vatican kulitambua taifa la Palestina.

Bwana Abbas anatarajiwa kuzungumza na Papa kuhusu wasiwasi kuwa rais mteule wa Marekani Donald Trump anapanga kuhamisha ubalozi wa Marekani nchini Israel kutoka Tel Aviv, na kuupeleka Jerusalem jambo ambalo Wapalestina wanasema, litaharibu uwezekano wa kupata makubaliano ya amani kufuatia majadiliano na Israel.

Swala la Jerusalem ni miongoni mwa maswala yanayovutia hisia kali na tata katika mzozo wote wa mashariki ya kati.

Palestina inalichukulia eneo la mashariki mwa Jeusalem kuwa mji wake mkuu wa taifa lake siku za usoni lakini Israel inalichukuwa eneo hilo lote kuwa mji wake mkuu.

Siku ya Jumapili Ufaransa itaandaa mkutano wa kimataifa mjini Paris ili kujaribu kuanzisha mazungumzo ya amani katika ya pande hizo mbili.