Mkutano kutatua mzozo kati ya Israel na Palestina wafanyika Ufaransa

Mkutano kati ya Israel na Palestina hujafanyika tangu 2014 Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mkutano kati ya Israel na Palestina hujafanyika tangu 2014

Mawaziri wa mashauri ya nchi za kigeni na wanadiplomasia wa zaidi ya mataifa sabini wanakutana mjini Paris, Ufaransa, kwa mkutano maalum kujadili mzozo na suluhu ya kudumu kati ya Israel na Palestina.

Hakuna wajumbe kutoka Israel au Palestina, ambao wanahudhuria mkutano huo.

Waandalizi kutoka Ufaransa, wanasema kwamba ni bora kuwekwa katika madaftari ya kumbukumbu, kwamba sulu katika mataifa hayo mawili, ni msingi wa siku zijazo wa muafaka wa amani.

Hayo yanatukia, licha ya msimamo mkali wa Marekani dhidi ya Israeli wakati ambapo Rais mpya Donald Trump anajiandaa kuchua uongozi.

Waziri mkuu wa Israeli, Bejamin Netanyahu, anaelezea mkutano huo kama mabaki ya kale.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wanajeshi wa Israel na Palestina hukabiliana mara kwa mara
Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mazungumzo ya amani yamekwama kutokana na ujenzi wa makaazi ya wayahudi