Adama Barrow apewa makao Senegal

Rais wa Senegal Macky Sall, amekubali kumpa makao bwana Barrow kwenye mji mkuu Dakar Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais wa Senegal Macky Sall, amekubali kumpa makao bwana Barrow kwenye mji mkuu Dakar

Ripoti kutoka chini Senegal zinasema kuwa rais mteule wa Gambia Adama Barrow atasalia nchini Senegal hadi wakati wa kuapishwa kwake wakati huu ambapo nchi ya Gambia inakumbwa na mzozo.

Shirika la habari nchini Senegal linasema kuwa rais wa nchi hiyo Macky Sall, amekubali kumpa makao bwana Barrow kwenye mji mkuu Dakar hadi pale atakapoapishwa tarehe 19 mwezi huu.

Rais wa sasa Yahya Jammeh amekataa kukubali kuwa alishindwa kwenye uchaguzi wa mwezi Disemba.

Siku ya Jumamosi rais wa Mali Ibrahim Boubacar Keita, alimtaka rais wa Gambia kuondoka madarakani ili kuzuia kuzuia umwagaji damu.

Alikuwa akizungumza wakati wa mkutano Afrika na Ufaransa kwenye mji mkuu wa Mali, Bamako, ambao ulitawaliwa na mzozo ulio nchini Gambia.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Rais wa sasa Yahya Jammeh amekataa kukubali kuwa alishindwa kwenye uchaguzi wa mwezi Disemba