Mfalme Kigeli azikwa Kigali

Mfalme Kigeli aliaga dunia mwezi Oktoba mwaka uliopita akiwa nchini Marekani
Image caption Mfalme Kigeli aliaga dunia mwezi Oktoba mwaka uliopita akiwa nchini Marekani

Mfalme wa mwisho nchini Rwanda ambaye alitawala katika kipindi kisichozidi mwaka mmoja kabla ya kukimbilia uhamishoni alizikwa jana Jumapili, eneo la Nyanza kusini magharibi mwa mji mkuu Kigali.

Nyanza ndio ulikuwa mji mkuu wa himaya ya ufalme.

Mfalme Kigeli aliaga dunia mwezi Oktoba mwaka uliopita akiwa nchini Marekani ambapo amekuwa akiishi tangu mwaka 1992.

Wengi wa wale waliohudhuria mazishi yake ni watu wa familia. Maafisa kutoka upande wa serikali walikuwa ni wachache.

Image caption Mfalme Kigeli aliaga dunia mwezi Oktoba mwaka uliopita akiwa nchini Marekani

Kwa sasa Rwanda ni Jamhuri na serikali ya sasa haitambui jamii ya kifalme na pia haitaki kuwapa umaarufu.

Wakati mfalme alikuwa hai aliripotiwa kuwa na matumaini kuwa angeweza siku moja kurudi Rwanda, lakini serikali ilisema kuwa ingemruhusu tu ikiwa angerudi kama raia wa kawaida.

Ufalme huo haukutaka Kigeli azikwe Rwanda ikiwa serikali ya sasa bado ilikuwa madarakani.

Hata hivyo mahakama moja nchini Marekani iliipa ushindi familia iliyokuwa nchini Rwanda ambayo ilitaka mwili wake kurudishwa ili kuzikwa.

Pia kuna mvutano ndani ya familia kuhusu ni nani atamrithi mfalme Kigeli.

Image caption Ufalme huo haukutaka Kigeli azikwe Rwanda ikiwa serikali ya sasa bado ilikuwa madarakani.

Mada zinazohusiana