Mtoto wa Barrow afariki baada ya kuumwa na mbwa

Bwana Barrow yuko nchini Senegal kabla ya kuapishwa siku ya Alhamisi. Haki miliki ya picha AFP/getty
Image caption Bwana Barrow yuko nchini Senegal kabla ya kuapishwa siku ya Alhamisi.

Mtoto wa kiume wa rais mteule wa Gambia Adama Barrow amefariki baada ya kuumwa na mbwa.

Habibou Barrow alifariki alipokuwa akipelekwa hospitalini kufuatia kisa hicho cha siku ya Jumapili, kilichotokea eneo la Manjai karibu na mji mkuu Banjul.

Mazishi yake tayari yashafanyika.

Bwana Barrow yuko nchini Senegal kabla ya kuapishwa siku ya Alhamisi.

Kwa mjibu wa ripoti hiyo, Barrow ana wake wawili na watoto wengine wanne.