Wabukala aidhinishwa kuwa mwenyekiti wa tume ya kupambana na rushwa Kenya

Rushwa limekuwa tatizo kubwa nchini Kenya
Image caption Rushwa limekuwa tatizo kubwa nchini Kenya

Askofu mstaafu wa kanisa la kianglikana nchini Kenya Eliud Wabukala, ndiye mwenyekiti mpya wa tume ya kupambana na ruswa nchini Kenya(EACC)

Uteuzi wa bwana Wabukala na Rais Uhuru Kenya uliidhinishwa na bunge Jumanne jioni.

Anachukua mahala pa Philip Kinisu, ambaye aliondolewa ofisini baada ya kutajwa kwenye kashfa ambayo ilikumba idara ya huduma kwa vijana.

Wakati wa kikao maalum cha bunge, wabunge waliunga mkono kwa wingi uteuzi wa Wabukala, wakiwa na matumaini kuwa askofu huyo mstaafu atakabiliana na mitandao ya ufisadi nchini Kenya.

Kiongozi wa wengi katika bunge la Kenya Aden Duale, amesema kuwa Wabukala anaingia katika tume hatari ambayo ufisadi hujipigania na ambayo wanyeviti wengine sita wameondoka bila kutekeleza lolote la kukabiliana na ufisadi.