Farasi ndio walisababisha vifo vingi zaidi Australia

Dr Ronelle Welton Haki miliki ya picha Paul Burston
Image caption Dr Ronelle Welton

Farasi waliwaua watu wengi zaidi nchini Austrralia miaka ya hivi karibuni kuliko nyoka wote wenye sumu kwa pamoja.

Daktari Ronelle Welton wa Chuo cha Melbourne anasema amechunguza takwimu za watu wanaolazwa hospitalini.

Kuanzia mwaka 2000 hadi 2013 farasi walisabasisha vifo vya watu 74.

Nyuki na wadudu wengine wa kuuma wanakuwa wa pili kama viumbe hatari zaidi, wakisababisha vifo 27 wakifuatiwa na nyoka ambao waliwaua watu 27.

Bui bui hawakusababisha vifo vyovyote wakati wa kipindi hicho.

Utafiti wa daktari Welton unapinga madai kuwa Australia ina wanyama wenye sumu kali.

Lakini kilichotia hofu ni kuwa watu wengi walitafuta matibabu hospitalini baada ya kuumwa na wadudu.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii