Italia: Watu 8 waokolewa kutoka jengo lililozikwa kwenye barafu

Helikopta Haki miliki ya picha AFP
Image caption Helikopta ziliitwa kwenye eneo la tukio mahala ambapo wmanusura walipatikana

Watu wanane wamepatikana wakiwa hai katika hoteli ya Italia-Rigopiano hotel, siku mbili baada ya kuzikwa katika theruji kubwa.

Waokoaji wanasema manusura hao sita wamebainika wakiwa wamezikwa chini ya theruji ,lakini walikuwa bado hawajaokolewa.

Mmoja wapo ni msichana mdogo, vimesema vyombo vya habari vya Italia.

" Wako hai na tunaongea nao," msemaji wa kikosi cha zima moto Luca Car alilieleza shirika la habari la Rheuters.

Barafu yenye kina kikubwa iliizika hoteli hiyo iliyopo eneo la mbali katika jimbo la kati la Abruzzo , baada ya matetemeko kadhaa ya ardhi kulikumba eneo hilo.

Takriban watu wanne wamethibitishwa kufa kwenye mkasa huo na wengine wapatao 20 hawajulikani walipo, huku juhudi za uokozi zikiendelea katika hali ngumu na mbaya ya hewa.

Haki miliki ya picha Hotel Rigapiano
Image caption Watoto wanaaminiwa kuwa miongoni mwa wageni waliokuwemo kwenye hoteli mkasa huo ulipotokea

Watoto wanaaminiwa kuwa miongoni mwa wageni waliokuwemo kwenye hoteli mkasa huo ulipotokea.

Timu za uokoaji zimekuwa zikiendelea na kazi ya kuwasaka manusura na miili ya wahanga wa mkasa huo kwa zaidi ya saa 24 huku kiwango cha joto kikiwa ni chini ya nyuzi joto sifuri.

Vikosi vya uokozi vimeomba usaidizi wa helikopta ili kuwaokoa watu wanane waliopatikana hai, kulingana na taarifa za vyombo vya habari vya Italia.

Haki miliki ya picha GETTY IMAGES / VIGILI DEL FUOCO
Image caption Hoteli ilikuwa imezikwa kabisa ndani ya barafu kwa saa kadhaa kabla timu ya waokoaji haijafika kwenye eneo la tukio reached the scene

Mnamo siku ya Jumatano matetemeko ya ardhi yakiwemo manne yenye ukubwa wa zaidi ya 5 kwa vipimo vya ritcha, yaliyokumba jimbo hilo ambalo tayari linakabiliwa na heruji nzito ambayo ilizika mifumo ya mawasiliani ya simu na kuharibu nyaya za umeme.

Milingoti ya simu ilianguka katika hoteli ya Rigopiano mapema Jumatano.

Baadhi ya taarifa zinasema kuwa wageni walikuwa wamekusanyika katika ukumbi wa chini wa gorofa ya hoteli wakisubiri kuokolewa kufuatia matetemeko ya ardhi.

Wamekaa kwa saa kwa saa 40 chini ya vifusi katika barafu na vifusi vya jengo.