Jammeh "kuachia madaraka na kuondoka"

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Bwana Jammeh alishindwa kwenye uchaguzi wa mwezi Disemba na mrithi wake Adama Barrow ameapishwa.

Kiongozi wa Gambia Yahya Jammeh atawachia madaraka na kuondoka nchini Gambia, kwa mujibu wa maafisa wanaongoza mapatano.

Wapatanishi wa Afrika Magharibi watliumia masaa kadha wakikutana na bwana Jammeh siku ya Ijumaa kuzungumzia hatma yake.

Msafara wa magari uliowabeba marais wa Guinea na Mauritania, umeondoka makao ya Jammeh lakini hayaaminiwi kuondoka nchi humo.

Gambia: Jammeh 'akubali kuachia madaraka'

Bwana Jammeh alishindwa kwenye uchaguzi wa mwezi Disemba na mrithi wake Adama Barrow ameapishwa.

Jammeh alikuwa amepewa makataa ya kuondoka madarakani kufikia saa sita mchana la sivyo aondolewe kwa nguvu na wanajeshi wanaoungwa mkono na UMoja wa Mataifa.