Waziri Mkuu wa Mauritius kumkabidhi mwanawe madaraka

Bwana Jugnauth amekuwa kwenye siasa za Mauritius kwa miongo kadha

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Bwana Jugnauth amekuwa kwenye siasa za Mauritius kwa miongo kadha

Waziri Mkuu wa Mauritius Anerood Jugnauth anasema anaoandoka madarakani na kumkabidhi mwanawe Pavind madaraka.

Waziri huyo mkuu mwenye umri wa miaka 82 alichukua wadhifa kwanza mwaka 1982.

Katika tangazo kwa njia ta runinga bwana Jugnauth anasema anajiuzulu ili kutoka nafasai kwa kiongozi mwenye umri mdogo na mwenye nguvu.

Mwanawe kwa sasa ni waziri wa fedha. Vyama vya upinzani vimekosoa hatua hiyo lakini hakuna kile vitafanya kuzuia hatua hiyo.

Jugnauth ni mkuu wa chama kikubwa ziadi katika muungano unaoongoza.

Mauritius, nchi iliyo habari Hindi ni koloni ya zamani ya Uingereza. Atakabidhi mwanawe madaraka Jumatatu asubuhi.