Uingereza: Tuna imani na silaha zetu za nuklia

Kombora lisilo na silaha likifanyiwa majaribio baharini
Maelezo ya picha,

Kombora lisilo na silaha likifanyiwa majaribio baharini

Wizara ya ulinzi nchini Uingereza inasema kuwa ina imani na silaha za nuklia za nchi hiyo licha ya ripoti ya kutokea hitilafu wakati wa majaribio.

Gazeti la Sunday Times, linasema kuwa kombora ambalo halikuwa limebeba silaha lililirushwa kutoka kwa manowari HMS Vengeance, karibu na pwani ya Florida mwezi Juni lilibadili mwelekeo na kuelekea nchini Marekani.

Majaribio ya awali yaliyofanikiwa yalikuwa yakitangazwa kwa hata kwa njia ya video, lakini jaribio hilo halikutangazwa.

Kimya hicho kilizua maswali kuhusu huenda kulikuwa na hililafu kabla ya kura ya bunge ya mwezi Julai, ambayo iliiamrisha kutolewa dola bilioni 50 za kuboresha mpango wa nyuklia wa Uingereza unaopitwa na wakati.

Maelezo ya picha,

Gharama ya kujenga manowari nne kwa sasa ni pauni bilioni 31