Wagonjwa wanavyoteseka kutokana na mgomo wa madaktari Kenya

Wagonjwa wanavyoteseka kutokana na mgomo wa madaktari Kenya

Ni zaidi ya mwezi mmoja sasa tangu madaktari nchini Kenya walipoanza kususia kazi, na hamna dalili za suluhu kupatikana.

Muungano wa madaktari umekataa kujadili tena makubaliano baina yake na serikali, ambapo walitunukiwa nyongeza ya asilimia mia tatu ya mshahara kando na maafikiano mengine ya kuboresha afya.

Mwandishi wetu Ferdinand Omondi alitembelea Hospitali Kuu la Eneo la Pwani, Mombasana kuandaa taarifa hii.