Wafungwa wengi waachiliwa Burundi

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mamia ya watu walikamatwa wakati wa maandamano ya kupinga muhula wa tatu wa Nkurunziza

Mamia ya wafungwa wameachiliwa kutoka magereza nchini Burundi kama njia ya kutekeleza msamaha wa rais uliatangazwa mwishoni mwa mwaka uliopita.

Wafungwa walioachiliwa ni pamoja na wanachama cha chama cha upinzani ambao walikamatwa karibu miaka mitatu iliyopita wakati polisi walikuwa wakizima maandamano mjini Bunjumbura.

Mmoja wao alitaka kuachilia kwa wafungwa wa kisiasa akisema kuwa si vizuri watu kufungwa kwa miaka mitatu bila sababu.

Maelfu ya watu wamekamatwa tangu mwezi Aprili mwaka 2015, kufuatia maandamano ya kupinga hatua ya rais Pierre Nkurunziza kuwania muhula wa tatu.

Kwa ujumla karibu watu 2500 watapata uhuru wao katika zoezi lililoanza siku ya Jumatatu.