Afya ya kiungo Mason yaimarika

Mason Haki miliki ya picha AP
Image caption Ryan Mason akiwa chini baada ya kugongana kichwa na beki wa Chelsea Gary Cahill

Mchezaji kiungo wa Hull City Ryan Mason afya yake imeimarika na anaweza kuongea baada ya jana kufanyiwa upasuaji wa fuvu la kichwa.

Mason aligongana kichwa na beki wa Chelsea Gary Cahill, katika dakika ya kumi na tatu ya mchezo wa ligi kuu England, na alipelekwa katika hospital ya St Mary's Hospital iliyoko jijini London, alikofanyiwa upasuaji huo.

Taarifa iliyotolewa na klabu ya Hull City kiungo huyu ataendelea kuwa chini ya usimamizi wa madaktari kwa siku kadhaa

Nahodha wa Hull City Michael Dawson, daktari wa timu Mark Waller, mkuu wa kitengo cha matibabu cha timu Rob Price, pamoja na mwenyekiti wa timu Matt Wild walimtembelea mchezaji huyo hospitalini.

Nao wachezaji wa Chelsea Gary Cahill, John Terry, na kocha msaidizi wao msaidizi Steve Holland alikwenda kumjulia hali mchezaji huyo.