Tillerson apita mchujo wa kwanza Marekani

Rex Tillerson Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rex Tillerson

Kamati ya Uhusiano na mataifa ya nje katika bunge la seneti la Marekani limepiga kura kwa tofuati ndogo kumuidhinisha Rex Tillerson aliyekuwa mkurugenzi wa kampuni kubwa ya mafuta Exxon Mobil, kuwa Waziri wa mambo ya nje.

Wanachama 11 wa Republican walimuunga mkono huku wabunge 10 wa Democratic wakimpinga.

Seneta wa chama wa cha Republican, Marco Rubio alimuunga mkono licha ya kuzozana na BwTillerson kuhusu uhusiano wake na Urusi.

Uteuzi huo sasa unawasilishwa katika bunge kamili la seneti.

Wakati huohuo Mike Pompeo ameapishwa kuwa mkurugenzi mkuu wa shirika la upelelezi CIA.