Jina la filamu ijayo ya Star Wars latangazwa

Felicity Jones na Diego Luna
Image caption Felicity Jones na Diego Luna wa filamu ya Rogue One

Jina la filamu mpya ya mwendelezo wa filamu za Star Wars limetangazwa, ambapo itaitwa Star Wars: The Last Jedi.

Katika taarifa kwenye mtandao wa Star Wars, watunga filamu hizo wamesema wako na mashabiki sugu wa filamu hizo na hata filamu nyingine na walitaka wawe wa kwanza kufahamu jina hilo.

''Kwa kuwashukuru mashabiki wetu, tunataka kuwafahamisha kwanza jina la sura inayofuata ya hadithi ya Skywalker ambayo itaitwa: STAR WARS: THE LAST JEDI.''

Makala ya 8 ya filamu hizo, - The Last Jedi - itazinduliwa rasmi mwezi Desemba.

Haki miliki ya picha Jonathan Olley/Lucasfilm
Image caption Rogue One: A Star Wars

Hakuna tole fupi la kuvumisha filamu hiyo lililotolewa kufikia sasa, lakini rais wa Lucasfilm Kathleen Kenndy, amedokeza kutakuwa na tangazo hilo katika majira yajayo ya kuchipua.

Watakaoigiza ni Daisy Ridley, John Boyega, Oscar Isaac, Anthony Daniels na Lupita Nyong'o .

Pia itamjumuisha hayati Carrie Fisher, kwani filamu hiyo ilikamilika mwaka jana kabla ya kifo chake .

Haki miliki ya picha Jonathan Olley/Lucasfilm

Filamu hiyo ya Last Jedi iliandikwa na kuelekezwa na Rian Johnson na maprodusa ni Kathleen Kennedy na Ram Bergman.

Wazalishaji wake wakuu ni J.J. Abrams, Jason McGatlin na Tom Karnowski.

Image caption Filamu za Star Wars zimekuwa maarufu sana duniani

Mada zinazohusiana