Anichebe kuwa nje ya dimba kwa wiki kumi

Anichebe Haki miliki ya picha Google
Image caption Victor Anichembe atakuwa nje ya uwanja kwa wiki kumi.

Mshambuliaji wa klabu ya Sunderland Victor Anichebe atakua nje ya dimba kwa wiki kumi akiuguza majeraha ya goti.

Anichebe mwenye umri wa miaka 28 alipata jeraha la goti muda mfupi baada ya kuingia uwanjani akitokea benchi katika mchezo wa timu yake dhidi ya West brom Albion.

Mchezaji huyu wa zamani wa Everton na West Brom ameifungia timu yake mabao matatu toka alipojiunga nayo mwezi Septemba mwaka jana.

Timu ya Sunderland iliyo chini ya kocha David Moyes kwa sasa imebakiwa na washambuliaji watatu tu ambao ni Jermain Defoe, Fabio Borini na kinda wa miaka 17 Joel Asoro.

Mchezaji mwingine wa Paka hao weusi Duncan Watmore atajua nje ya uwanja kwa msimu mzima akisumbuliwa na goti.