Trump: Tutajenga ukuta katika mpaka na Mexico

Ukuta utakaojengwa katika mpaka wa Marekani na Mexico Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Ukuta utakaojengwa katika mpaka wa Marekani na Mexico

Rais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa siku kuu kuhusu usalama wa Marekani imepangwa ikiwemo tangazo la kujenga ukuta kati ya Marekani na Mexico.

Donald Trump amesema kuwa ujenzi wa ukuta mrefu wa wenye maili 2000 katika mpaka wa Mexico ni miongoni mwa mapendekezo yake wakati wa kampeni za urais.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Rais Donald Trump wa Marekani na mkewe Melanie

Kutakuwa na mikakati ambayo pia italazimu miji mitakatifu nchini Marekani kushirikiana na mamlaka katika kuwarejesha makwao wahamiaji haramu.

Miji mitakatifu ni maeneo ambayo hayawakamati ama kuwazuilia wahamiaji wanaoishi katika taifa hilo kinyume na sheria.

Mada zinazohusiana