Southampton yatinga fainali EFL

Saint Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wachezaji wa Southampton wakishangilia goli

Timu ya Southampton ama watakatifu wametinga katika hatua ya fainali ya michuano ya kombe la ligi nchini England (EFL).

Watakatifu hao wametinga hatua hiyo baada ya kuichapa Liverpool kwa bao 1-0 katika mchezo wa nusu fainali ya mkondo wa pili mchezo ulifanyika katika dimba la Anfield .

Bao pekee lililoipa timu hiyo ushindi liliwekwa kambani na mshambuliaji Shane Long katika dakika za lala salama za mchezo huo.

Katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza Liverpool walifungwa kwa bao moja kwa bila hivyo Southampton wanawaondosha kwa jumla ya mabao 2-0.

Nusu fainali nyingine ya pili inachezwa leo hii ambapo Hull City watakua wenyeji wa Manchester United katika mchezo wa kwanza United walishinda kwa mabao 2-0 .

Mchezo wa fainali utafanyika tarehe 26/2 mwaka huu katika uwanja wa Wembley