Mlipuko wa Ugonjwa wa Manjano Brazil, vifo vyaongezeka

Brazili kupambana na ugonjwa wa manjano Haki miliki ya picha EPA
Image caption Brazili kupambana na ugonjwa wa manjano

Maafisa nchini Brazil wameamuru kufanyika kwa takriban chanjo milioni 11 na nusu ya homa ya manjano.

Taifa hilo kwa sasa linakabiliwa na mlipuko mkubwa wa ugonjwa huo.

Wizara ya afya nchini humo imethibitisha wagonjwa 70 wa ugonjwa huo na vifo vya watu 40 katika maeneo ya mashambani katika jimbo la Minas Gerais.

Mamia ya wagonjwa wamekuwa wakichunguzwa kama wameambukizwa na ugonjwa huo.