Al-Shabab lawaua wapelelezi wa Marekani na Kenya

Wapiganaji wa kundi la Al-Shabab Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wapiganaji wa kundi la Al-Shabab

Wapiganaji wa kundi la al-Shabab nchini Somalia wamewaua watu 3 inaowatuhumu kwa kulipelelezea shirika la ujasusi nchini Marekani CIA pamoja na vitengo vyengine kulingana na tovuti ya Somali Memo inayounga mkono kundi hilo.

Watatu hao waliuawa mbele ya kundi kubwa la watu kusini magharibi mwa mji wa Yaq-Barawe.

Abdullahi Damey Mohamud Nur mwenye umri wa miaka 36 alipatikana na hatia ya kulichunguzia kundi la CIA kutoka Marekani ambapo alikuwa akipokea mshahara wa dola 200 kila mwezi, kulingana na mtandao huo.

Al-Shabab lakiri kuvamia kituo cha polisi Kenya

Shambulio la hoteli lawaua watu 12 Somalia

Watu 15 wauawa kwa bomu Somalia

Jaji wa al-Shabab alisema kuwa Mohammed alikiri kuwasaidia Marekani kwa kutekeleza mashambulio kwa kutumia ndege zisizo na rubani.

Jaji huyo pia alisema kuwa Mohamed Iman Hassan mwenye umri wa miaka 42 aliuwawa kwa kupelelezea Kenya na alikuwa akipata dola 150 kama mshahara.

Mohamed Sharrif Ali mwenye umri wa miaka 21,alituhumiwa kwa kuisaidia mamlaka ya Jubbaland kukusanya habari kuhusu kundi hilo.