Moto wa nyika waangamiza mji Chile

Santa Olga Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mjini Santa Olga, nyumba 1,000 zimeteketea kabisa

Mataifa yameanza kutuma wazima moto nchini Chile kusaidia taifa hilo kukabiliana na moto mbaya zaidi katika historia ya taifa hilo.

Urusi imetuma ndege yenye uwezo wa kubeba tani kadha za maji kujaribu kusaidia kuzima moto huo wa nyika.

Moto huo umeenea kwa kasi sana maeneo ya kati ya Chile, ambapo unasaidiwa na upepo mkali, kiwango cha juu cha joto na hali kwamba maeneo hayo yamekabiliwa na kiangazi kwa muda.

Mji Santa Olga, unaopatikana kilomita 240 kusini mwa Santiago umeharibiwa kabisa na moto huo.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mwiili wa mtu mmoja uliokuwa umeteketea ulipatikana katika mji wa Santa Olga. Watu 6,000 walifanikiwa kutoroka bila majeraha.
Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wakazi walitoroka wakiwa na wanyama wao. Hapa, wakazi wanaonekana ndani ya gari, farasi wao akikimbia kuandamana nao nje
Haki miliki ya picha AFP
Image caption Watu wengi wameacha bila makao na bila matumaini
Haki miliki ya picha AFP
Image caption Moto huo umeteketeza karibu hektari 238,000 (ekari 588,000) kote nchini Chile. Maafisa wa msitu wanasema moto huo unaendelea kuenea
Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wazima moto wamekuwa wakiombolewa wenzao watano waliofariki wakikabiliana na moto huo na kuwaokoa wakazi

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii