Tanzania yatahadharisha wahalifu waliotoka Burundi
Huwezi kusikiliza tena

Tanzania yatahadharisha 'raia wahalifu' waliotoka Burundi

Serikali ya Tanzania imeonya kuwa itabatilisha uraia wa waliokua wakimbizi wa Burundi wanaoishi katika kambi ya Ulyankulu katika wilaya ya Kaliua mkoani Tabora, ikiwa itathibitisha kuwa wanahusika katika vitendo vya uhalifu.

Raia hao walipatiwa uraia baada ya kuishi nchini humo kwa miaka mingi.

Eneo linalozunguka maeneo hayo linadaiwa kuwa na uhalifu mwingi zaidi kuliko eneo lingine lolote nchini humo na silaha nyingi haramu zimekamatwa katika eneo hilo zikiwa na usajili wa nchi jirani hususani Burundi.

Aidha Tanzania imesema imebadilisha utaratibu wa kuwapokea wakimbizi kwa makundi badala yake kila mmoja atapekuliwa kwa umoja wake.

Arnold Kayanda amefanya mazungumzo na Waziri wa mambo ya ndani nchini Tanzania Mwigulu Nchemba.

Mada zinazohusiana