Tofauti kati ya ukuta wa Trump na kuta zingine maarufu zilizojengwa

Mpaka kati ya Mexico na Marekani
Image caption Mpaka kati ya Mexico na Marekani

Rais wa Marekani Donald Trump ameapa kuendelea na mipango yake ya kujenga ukuta wa urefu wa kilomita 3000 kwenye mpaka kati ya Marekani na Mexico.

Ukuta huo utakuwa na urefu wa kati ya mita 9 na 16 na utajengwa kwa kutumia changarawe.

Warepublican na wafuasi wao wanasema kuwa ukuta huo utawazui raia wa Mexico wanaoingia Marekani kinyume na sheria.

Tayari kuna ua kwenye mpaka kati ya Mexico na Marekani.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Sehemu moja kwenye ua kati ya Marekani na Mexico walinzi uruhusu watu kuongea na marafiki zao na jamaa

Kuna kuta nyingi katika historia ambazo zilijengwa na kutenganisha mataifa. Lakini zinafananishwa vipi na mpango wa ukuta kati ya Marekani na Mexico.

Ni miaka 27 iliyopita tangu ukuta wa Berlin kubomolewa.

Tutaanza na ukuta wa Berlin:

Kwa hili tutaangazia nyuma miaka ya 1950 wakati Ujerumani iligawanyika pande mbili, Mashariki na Magharibi.

Haki miliki ya picha BBC Newsround
Image caption Ujerumani Magharini na Mashariki zilitenganishwa na ukuta wa Berlin

Wakaazi wa upande uliodhibitiwa na Ufaransa, Uingereza na Marekani wa Magharibi, waliamka siku moja mwezi Agosti mwaka 1961, na kupata ukuta kati yao na eneo lililokuwa likidhibitiwa na muungano wa kisovieti.

Mwanzo ulikuwa ni ua tu lakini baadaye ulijazwa na changarawe yenye urefi wa mita 3.6 sehemu zingine.

Ulikuwa na umbali wa kilomita 100 na ua wa kilomita 66.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Ukuta wa Berlin

Ukuta wa Trump utakuwa na umbali mkubwa lakini si katika historia.

Mpaka kati ya Mareknia na Mexico una umbali wa kilomita 3000

Kwa hivyo ikiwa Trump atauzungusha sehemu kama za milima, atakuwa na changamoto za kuufana mrefu zaid kuliko ukuta wa China.

Image caption Ukuta mrefu zaidi

Umbali kamili wa ukuta wa China haujulikani lakini inaaminiwa kuwa wakati mmoja ulikuwa na umbali wa kilomita 20,000.

Una urefu wa hadi mita saba sehemu zingine

Haki miliki ya picha Thinkstock
Image caption Ukuta wa China

Lakini ukuta wa Trump unaweza kushinda kuta zingine kwa urefu.

Trump hawezi kuamua ukuta huo unaweza kuwa na urefu wa kiasi gani, lakini ameshatamka urefu wa mita 16. Huo utakuwa urefu wa zaidi ya basi tatu.

Image caption Ukuta mrefu zaidi

Ukuta wa Hadrian ambao ulijengwa kwa amri ya Emperor Hadrian mwaka wa 122AD, ulikuwa na urefu wa basi.

Ulikuwa na umbali wa kilomita 117 na ulikuwa ukitenganisha England na Scotland.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Ukuta wa Hadrian

Mada zinazohusiana