Mkuu wa magereza akamatwa akitoroka Gambia

Ramani ya inayoonyesha mataifa ya Gambia Senegal na Guinea Bissau
Maelezo ya picha,

Ramani ya inayoonyesha mataifa ya Gambia Senegal na Guinea Bissau

Maafisi wa polisi nchini Senegal wanasema kuwa wamemkamata mkuu wa magereza nchini Gambia Jenerali Bora Colley alipojaribu kuvuka na kuelekea Guinea Bissau.

Taarifa ya polisi inasema kuwa alikamatwa siku ya Jumatano na baadaye kukabidhiwa jeshi la Senegal.

Makundi ya haki za kibinaadamu yanasema kuwa kiwango kikubwa cha ukandamizi ulifanywa chini ya uongozi wa aliyekuwa rais wa taifa hilo Yahya Jammeh ikiwemo mateso pamoja na mauaji ya kiholela ambayo yalifanyika katika jela.

Senegal ilichukua jukumu muhimu la kumsihi rais Yahya Jammeh kuondoka nchini humo siku ya Jumamosi.