Mbunge apendekeza bima kwa wanywaji pombe Kenya

Mbunge apandekeza bima kwa wanywaji pombe Kenya Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mbunge apandekeza bima kwa wanywaji pombe Kenya

Mbunge mmoja nchini Kenya amewasilisha mswada bungeni kuzishinikiza kampuni zinazouza pombe kutoa asilimia ndogo ya faida yao kuwadhamini wanywaji ambao wataathirika na pombe hiyo.

Mbunge Gideon Mwiti anataka watengenezaji wa pombe kutoa kati ya asilimia 5 na 10 ya mapato wanayopata kwa kampuni za bima ili kuwafidia watu ambao wataathirika na pombe ama hata kupata ajali kwa kuwa walevi kulingana na gazeti la Daily Nation nchini humo.

Mswada huo pia unapendekeza kwamba iwapo mtu atafariki kutokana na athari za kunywa pombe ,kampuni hizo za pombe zilazimike kufidia familia yake.

Bw Mwiti pia amezishutumu kampuni za pombe kwa kushindwa kukuza pombe zisizo na madhara kwa afya, kwa mujibu wa ripoti hiyo.