Jaji apiga marufuku amri ya Trump kurudisha wahamiaji makwao

Donald Trump Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Donald Trump

Mahakama moja ya New York imeridhia ombi la wanaharakati waliokwenda mahakamani kupinga amri za Rais Trump za kupiga marufuku wakimbizi wa Syria na raia wengine wa nchi sita za kiislamu kwamba wasiingie marekani, mionongi mwao nchi za Iran, Iraq, Somalia, Sudan, Libya na Yemen.

Sasa koti hiyo imeamuru wote waliozuiliwa kupitia amri hizo waachiwe .

Tayari kuna ripoti kutoka uwanja wa ndege wa John F Kennedy kwamba watu kadhaa wamezuiwa kuingia Marekani wakiwemo wale ambayo walikuwa wamepewa ruhusa kwenda kuishi marekani kupitia mpango wa green card.

Waandamanaji kwa upande wao waliokuwa uwanjani hao walipaaza sauti kusema 'let them in' yaana kutaka watu hao waruhisiwe kuingia.