Merkel alaani vikwazo vya Trump

Angela Merkel Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Angela Merkel

Kiongozi wa Ujerumani, Angela Merkel, amelaani vikwazo vilivyowekwa na Rais wa Marekani Donald Trump kukataza kupokea wasafiri kutoka nchi zenye wa Islamu wengi.

Msemaji wa Bibi Merkel, Steffen Seibert, alieleza kuwa Bibi Merkel, haamini kuwa vita dhidi ya ugaidi, vinastahiki kuwatilia shaka kwa jumla, watu wa asili au dini fulani.

Meya wa London, Sadiq Khan ambaye ni Muislamu alielezea amri hiyo ya marufuku kuwa ya aibu na ya kikatili.

Alisema sera hiyo mpya, inakwenda kinyume na maadili ya uhuru na uvumilivu, ambayo ndiyo misingi iliyojenga taifa la Marekani.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii