Amri ya Trump: Ni nani anaathirika?

Maandamano yalifanyika kwenye miji mingi Marekani Haki miliki ya picha AFP
Image caption Maandamano yalifanyika kwenye miji mingi Marekani

Uamuzi wa rais wa Marekani Donald Trump wa kuwazuia wahamiaji na kuwapiga marufuku kwa muda watu kutoka nchi saba za kiislamu imezua maandamano kote nchini na kuzua shutuma kutoka kote duniani.

Wengine wanaitaja amri hiyo kama ahadi ya kampeni ya Trump ya kuifanya Marekani kuu tena.

Lakini amri hiyo ni gani, iliyopewa jina "marufuku kwa waislamu" na wale wanaoipinga.

Haya ni baadhi ya mambo makuu kwenye amri hiyo.

Ni kipi kinafanyika?

  • Amri hiyo inapiga marufu mpango wa wakimbizi wa Marekani kwa muda wa siku 120.
  • Pia kutakuwa na marufuku kwa wakimbizi wa syria.
  • Na yeyote ambaye anawasili kutoka nchi saba zenye waislamu wengi zikiwemo Iraq, Syria, Iran, Libya, Somalia, Sudan, na Yemen wanakabiliwa na marufuku ya siku 90.
Image caption Nchi ambazo amri hiyo inalenga
  • Amri hiyo pia inatoa idadi ya wakimbizi ambao watakubalika mwaka 2017 ya 50,000 kinyume na ya awaliaya wakimbizi 110,000 iliyotangazwa na Raia wa zamani Barack Obama.

Wasafiri wote walio na uraia au uraia mara mbili kutoka Iran, Iraq, Libya, Somalia, Sudan, Syria na Yemen hawaruhusiwi kuingia Marekani kwa muda wa siku 90 na kupewa visa.

Hawa ni pamoja na wale walio na uraia mara mbili na nchi washirika ikiwemo uingereza, licha ya Canada kufahamishwa kuwa wale walio na uraia wa nchi hiyo hawataathiriwa.

Image caption Majimbo yaliyo kwenye mipaka ya Marekani

Itakuwaje kwa watu wenye green card?

Mkuu wa ikulu ya White House Reince Priebus anasema kuwa walio na green card hawataathiriwa lakini alikiambia kituo cha NBC kuwa watahojiwa vikali katika viwanja vya ndege.

Afisa mmoja wa cheo cha juu katika idara ya usalama wa ndani aliiambia CNN kuwa hakuna mtu mwenye green card aliyezuiwa kuingia Marekani hadi Jumapili jioni.

Trump anasema nini?

Bwana Trump anasema marufuku kwa mpango wa wakimbizi ulihitajika ili kuyapa mashirika ya serikali muda ya kubuni mfumo mgumu wa ukaguzi na kuhakikisha kuwa visa hazitolewi kwa watu walio tisho kwa usalama wa nchi.

"Hii si marufuku ya waislamu, jinsi vyombo vya habari vinaripoti," Rais alitoa taarifa iliyotolewa kupitia Facebook.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Amri hiyo ya Trump imekosolewa vikali na makundi ya haki

Inatekelezwa kwa njia gani?

  • Kumekuwa na hali ya kukanganya. Jaji alitoa amri ya kusitishwa kwa muda kufukuzwa watu walio na visa au wakimbizi waliokuwa kwenye viwanja vya ndege vya Marekani. Inakadiriwa kuwa kati ya watu 100 na 200 wameuzuliwa katika viwanja vya ndege.
  • Wasafiri wamezuiwa kupanda ndege zinazoenda Marekani. Pia kuna ripoti kuwa wahudumu wa ndege walizuiwa kuingia nchini Marekani.
  • Licha ya madai kuwa wale walio na green Card kutoka nchi hizo saba hawataathiriwa, maafisa wanasema kuwa wale waliokuwa nje ya Marekani wakati amri hiyo ilipotangazwa lazima wakaguliwe kabla ya kuruhusiwa kuingia Marekani.
Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Maandamano yalifanyika kwenye viwanja vya ndege

Wakosoaji wanasema nini?

Makundi ya haki za binadamu yanasema kuwa amri hizo za Trump zinawalenga waislamu kutokana na imani yao na wataikabili kisheria amri hiyo. Pia wanasema kuwa hakuna wakimbizi ambao wamepatikana na hatia ya kuhusika na ugaidi.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Kati ya wakimbizi 84,995 walioingia nchini Marekani mwaka 2016, 12,486 walitoka nchini Syria.