Israel yaishtumu Iran kwa kujaribu kombora lake

Israel imeishtumu Iran kwa kukiuka maamuzi ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kwa kufanyia majaribio kombora lake la masafa ya kadri
Image caption Israel imeishtumu Iran kwa kukiuka maamuzi ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kwa kufanyia majaribio kombora lake la masafa ya kadri

Israel imeishtumu Iran kwa kukiuka maamuzi ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kwa kufanyia majaribio kombora lake la masafa ya kadri

Waziri mkuu nchini humo Benjamin Netanyahu amesema kuwa jaribio hilo la kombora la masafa ya kadri ni ukiukaji wa sheria za Umoja wa Mataifa.

Amesema kuwa atapigania Iran kuwekewa vikwazo vipya vya kimataifa wakati wa ziara yake mjini Washington mwezi ujao.

Maafisa wa Marekani wamethibitisha kufanyika kwa jaribio hilo la kombora lakini wakasema kuwa haijabainika iwapo lilikiuka sheria za Umoja wa Mataifa iliopitishwa 2015 kufuatia mpango wa kimataifa kuuwekea vikwazo mpango wa Nuklia wa Iran.

Hakujakuwa na tamko lolote kutoka Iran.

Kabla ya kuchukua mamlaka ,rais Trump alitaja mpango huo wa Iran kuwa hatari kubwa na kusema kuwa atasitisha majaribio yake ya makombora.