Israel kujenga makaazi 3000 zaidi huko West Bank

Makaazi mapya ya Israel yaliopo katika eneo la West Bank Haki miliki ya picha AFP
Image caption Makaazi mapya ya Israel yaliopo katika eneo la West Bank

Taifa la Israel limetengaza mipango ya kujenga makaazi 3000 zaidi katika ene la West Bank .

Hatua hiyo inajiri baada ya serikali kuidhinisha ujenzi wa nyumba 2500 na nyengine 100 zaidi mashariki mwa Jerusalem.

Wapalestina wanadai umiliki wa maeneo yote mawili.

Awali jeshi la Israel lilikuwa linajiandaa kutekeleza operesheni ya agizo la mahakama ya kuwandoa walowezi waliojenga katika eneo la Amona katika eneo la West bank.

Siku ya Jumatatu wakaazi walipewa makataa ya saa 48 kuondoka.

Walowezi hao waliokuwa wamejenga katika ardhi ya Palestina .