Rais wa Angola Eduardo dos Santos kustaafu mwaka huu

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Waziri wa ulinzi nchini Angola Joao Lourenco

Waziri wa ulinzi nchini Angola Joao Lourenco, mwenye umri wa miaka 62, atakuwa mgombea wa urais wa chama cha MPLA kwenye uchaguzi wa mwezi Agosti, kwa mujibu wa rais wa nchi hiyo Eduardo dos Santos.

Bwana Dos Santos mwenye umri wa miaka 74 amethibitisa kuwa ataondoka madarakani baada ya kuitawala nchi kwa kipindi cha miaka 38, katika taifa hilo lenye utajiri wa mafuta na almasi.

Amelaumiwa kwa utawala wa kiimla baada ya kumteua bintiye Isabel dos Santos kama mkuu wa kampuni ya mafuta ya serikaki Sonangol.

Alitajwa na jarida la Forbes kama mwanamke tajiri zaidi barani Afrika akiwa na mali ya thamani ya dola bilioni 3.3.

Waakilishi wa Bi Santos wanakana madai kuwa utajiri wake umetokana na wadhifa wa babake kama rais wa Angola.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais Eduardo dos Santos ametawala kwa miaka 38