Mkewe El Chapo akatazwa kumuona mumewe

El Chapo Guzman katikati Haki miliki ya picha Reuters
Image caption El Chapo Guzman katikati

Mlanguzi mkuu wa madawa ya kulevya, raia wa Mexico, Joaquin Guzman, amelalamika alipofikishwa mahakamani mjini New York, akisema kuwa anazuiliwa kwa njia isiyofaa katika gereza moja la Marekani.

Guzman, ambaye amefanikiwa kutoroka mara mbili kutoka magereza ya Mexico, aliwahi kutoroka kupitia kikapu kikubwa na mara ya pili alichimba shimo kubwa chini ya ardhi kupitia seli yake. Hivi sasa anazuiliwa akiwa pekee katika gereza lenye ulinzi mkali jijini New York.

Mawakili wake wanasema kuwa mkewe amezuiliwa kumtembelea tangu asafirishwe chini ya ulinzi mkali kutoka Mexico mwezi uliopita.

Haki miliki ya picha AFP/getty Images
Image caption Mkewe El Chapo Guzman

Wakati mwingi Guzman haruhusiwi kutangamana na wafungwa wengine.

Guzman anashtakiwa kwa kuwa na silaha kinyume cha sheria ya ulagunzi wa madawa ya kulevya.