Rais wa Liberia apiga marufuku safari za kigeni

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf

Rais wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf ametangaza marufuku ya siku 60 kwa safari za nje ya nchi kwa maafisa wa serikali ambayo inaanza mwezi huu wa Februari.

Taarifa iliyotolewa siku ya Jumamosi, ilisema kuwa wale ambao wameathiriwa na marufuku hiyo ni pamoja na wakuu wa wizara, mashirika, makimishina pamoja na manaibu wao.

Wale ambao watahitaji kusafiri wataomba ruhusa kutoka kwa rais mwenyewe, ni ikiwa tu itabainika kuwa safari hiyo itakuwa ya manufaa kwa nchi.

Taarifa hiyo haikutoa sababu ya kuchukuliwa kwa hatua hiyo, lakini waandishi wa habari wanasema kuwa hifadhi ya sarafu za kigeni nchini Liberia ni ndogo mno, kutokana na kushuka kwa bei ya bidhaa za nchi hiyo.