Wapenzi 3 wa jinsia moja watakiwa kuripoti polisi Tanzania

Wapenzi wa jinsia moja
Image caption Wapenzi wa jinsia moja

Mamlaka nchini Tanzania imewataka watu watatu inaowashutumu kwa kuwa wapenzi wa jinsia moja kuripoti kwa maafisa wa polisi ili kuhojiwa la sivyo wakamatwe.

Naibu waziri wa afya nchini humo Hamis Kingwangalae amesema kuwa watatu hao walikuwa wakisambaza harakati za wapenzi wa jinsia moja kupitia mitandao ya kijamii kinyume na sheria.

Vitendo vya wapenzi wa jinsia moja ni kinyume na sheria nchini Tanzania na walio na hatia hupewa adhabu ya kifungo cha hadi miaka 30 jela .

Mwaka uliopita ,waziri wa afya alitangaza kwamba mpango wa kuwapatia matibabu wapenzi wa jinsia moja walio na virusi vya HIV utasimamishwa.

Serikali pia imetishia kupiga marufuku makundi ambayo yanaunga mkono haki za watu wa mapenzi ya jinsia moja.