Mafuta ya kupanga uzazi kwa wanaume yafaulu majaribio

Mbegu ya kiume Haki miliki ya picha SCIENCE PHOTO LIBARY
Image caption Mbegu ya kiume

Mafuta yanayotumiwa na wanaume katika mpango wa uzazi yamefaulu, baada ya kufanyiwa majaribio kwa tumbili.

Majaribio ya mafuta hayo mapya yanayozuia mbegu za kiume kuingia kwa pamoja na mafuta hayo, yamefanyiwa majaribio kwa tumbili na kuonekana kufaulu.

Mafuta hayo yaitwayo Vasalgel, yanatumika kama kizuizi, mara inapodungwa ndani ya mishipa ya kupitishia mbegu za kiume kwenye uume wa mwanamume.

Mpango wa uzazi kwa wanaume

Haki miliki ya picha Science Photo Library
Image caption Ukataji wa mshipa wa kupitishia mbegu ya kiume ya uzazi, huwa ni tendo la kudumu, licha ya kuwepo kwa wanaume ambao hufanyiwa operesheni ya kurejesha tena hali hiyo

Kampuni inayoshughulikia hilo, inasema kuwa majaribio hayo yaliyodumu miaka miwili iliyopita, na kuchapishwa katika jarida la Basic and Clinical Andrology, yanaonyesha kuwa kuwa mafuta hayo yanafanya kazi na ni salama kwa wanyama wanaofanana na binadamu.

Majaribio kwa Tumbili yafaulu

Haki miliki ya picha CALIFORNIA NATIONAL PRIMATE RESEARCH CENTRE
Image caption Hakuna tumbili yeyote wa kiume aliyetumia mafuta hayo, alifaulu kummzalisha tumbili wa kike

Inaleta matumaini kuwa na ushahidi tosha, kuanza kufanyiwa majaribio kwa wanaume wa kibinadamu katika kipindi cha miaka michache ijayo.

Ikiwa mradi huo utapata fedha za msaada, bila shaka utawasaidia wanaume wengi duniani kujumuika ipasavyo katika hali ya mpango wa uzazi.