Al-Shabab washambulia kikosi cha AU Somalia

Al-shabab ni tisho Afrika Mashariki Haki miliki ya picha AP
Image caption Al-shabab ni tisho Afrika Mashariki

Kundi la wanamgambo wa kiislamu nchini Somalia la al-Shabab, limeshambulia msafara wa kikosi cha Muungano wa Afrika kilicho nchini humo.

Shambulizi hilo lilitokea karibu na mji wa Mahadaay kati kati mwa eneo la Shabelle karibu kilomita 120 kaskazini mwa mji mkuu Mogadishu.

Wenyeji waliiambia idhaa ya kisomali ya BBC, kuwa mapigano ya kutumia silaha kubwa yaliendelea kwa karibu saa moja, lakiniki hakuna ripoti za maafa.