Al-Shabab washambulia wanajeshi wa AU nchini Somalia

Al-Shabab washambulia wanajeshi wa AU nchini Somalia

Wapiganaji wa Kundi la Al shabab nchini Somalia limeshambulia msafara wa vikosi vya kulinda amani vya AMISOM nchini humo. Shambulio hilo limetokea karibu na mji wa Mahadaay katika jimbo la Shabelle, kilometa ishirini kaskazini mwa mji mkuu Mogadishu.

Wenyeji wanasema mapigano ya kutumia silaha nzitonzito yaliendelea kwa karibu saa moja. Hakuna vifo vilivyoripotiwa. Wabunge na wale wa bunge kuu wanajiandaa kupiga kura hapo kesho kumchagua Rais huku kukiwa na ulinzi mkali.

Sehemu kadhaa za Mogadishu ziko katika hali ya hatari, magari hayaruhisiwi kutembea na ndege haziruhusiwi kufanya safari zake.

Mwandishi wetu Ferdinand Omondi yuko mjini Mogadishu.