Wanawake kugoma kumpinga Trump Marekani

Picha zilizoachwa karibu na White House wakati wa maandamano ya Januari 21 Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Picha zilizoachwa karibu na White House wakati wa maandamano ya Januari 21

Waandalizi wa maandamano ya wanawake wa mji wa Washington ya kumpinga Rais Donald Trump, wanapanga mgomo wa wanawake.

Akaunti yao ramsi ya twitter ilitangaza habari za mpango huo.

Ilijumuisha picha inayosema "siku isiyo na wanawake"

Mgomo huo unafuatia maandamano makubwa katika historia ya Marekani mjini washington tarehe 21 mwezi Januari huku mamilioni ya watu wakiandamana kwa uzalendo kote duniani.

Mgomo mwingine tayari ulikuwa umepangwa nchini Marekani tarehe 17 mwezi Februari na kundi linalojiita Strike4Democracy kumpinga Trump.

Terehe ya mgomo huo wa wanawake ilitangazwa baadaye.

Waandalizi wanasema pia kuwa wanaunga mkono majaribio ya makundi mengine kugoma yakitumia nguvu za kiuchumi.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Maandamano ya wanawake mjini Washington

Kipi kitatokea wakati wanawake watagoma?

Hatua ya wanawake kugoma ina historia yake ya kuangazia kutokuwepo usawa kwenye majukumu ya nyumbani.

Wanawake wa Iceland waligoma mwaka 1975 na kuwaacha waume zao wakiwatunza watoto, wakipika na kufanya usafi.

Miaka mitano baadaye nchi hiyo ilimchagua kiongozi mwanamke wa kwanza aliyechaguliwa kidemokrasia.

Mwaka uliopita wanawake nchini Poland nao waligoma kupinga sheria za utoaji mimba zilizopendekezwa na serikali.