Mahakama yakataa kurejesha marufuku ya Trump

Mama na bintiye katika uwanja wa ndege wa Los Angeles Haki miliki ya picha AP

Mahakama ya Rufaa nchini Marekani imekataa kuirudisha tena marufuku iliyowekwa na Rais wa Marekani Donald Trump ya wasafiri kutoka nchi saba za kiislamu na Wakimbizi wote kuingia nchini Marekani.

Jopo la majaji watatu limepinga kwa kauli moja kubadilisha uamuzi uliotolewa na jaji wa jimbo la Washington ambaye wiki iliyopita alizuwia sehemu ya amri iliyotolewa na rais.

Bwana Trump amesema kuwa ulikuwa ni uamuzi wa kisiasa na hatimaye itapitishwa.

Mada zinazohusiana