Afrika kwa Picha Wiki Hii: 3-9 Februari 2017

Mkusanyiko wa picha za kuvutia zaidi za matukio kutoka kote barani Afrika wiki hii.

Mogadishu, Somalia - 9 Februari 2017 Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wanawake nchini Somalia waimba na kusherehekea kuchaguliwa kwa Mohamed Abdullahi 'Farmajo' kuwa rais wa nchi hiyo mjini Mogadishu Alhamisi...
Mogadishu, Somalia -9 Februari 2017 Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wabunge walimchagua rais huyo chini ya ulinzi mkali katika uwanja wa ndege siku moja awali...hapa, wakazi wa Mogadishu wanaonekana wakishangilia wakiwa juu ya gari.
Libreville, Gabon - 5 Februari 2017 Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Simba Wasiofungika wa Cameroon nao waliibuka mabingwa wa soka Afrika Jumapili. Mashabiki hapa wanaonekana kabla ya mechi ya fainali dhidi ya Misri mjini Libreville, Gabon.
Rokia Traore Libreville, Gabon - Jumamosi 4 Februari 2017 Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mwanamuziki wa Malia Rokia Traore alikuwa miongoni mwa nyota wachache wa muziki Afrika Magharibi waliotumbuiza wakati wa sherehe ya kufunga rasmi michuano hiyo ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) siku moja awali.
Buthuel Buthelezi, Johannesburg, 4 Februari 2017 Haki miliki ya picha AP
Image caption Siku hiyo tu, katika jiji la Johannesburg, Afrika Kusini, afisa wa uwanja anaonekana akitumia kifaa cha kuzima moto kuwafukuza nyuki waliochelewesha mechi ya kriketi kati ya Afrika Kusini na Sri Lanka.
Anyama, Ivory Coast - Tuesday 7 February 2017 Haki miliki ya picha EPA
Image caption Mfanyakazi hapa anaonekana akitenganisha kokwa za kola katika mji wa Anyama, Ivory Coast Jumanne. Ivory Coast ndiyo nchi ya pili kwa uzalishaji wa kola duniani.
Mfuasi wa Muhammadu Buhari Jumatatu 6 Februari, 2017 Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mwendesha huyu wa baiskeli ya magurudumu matatu mjini Abuja, Nigeria aliamua kutumia njia ya kipekee kumuunga mkono Rais Muhammadu Buhari Jumatatu. Buhari yupo Uingereza kwa matibabu.
Sabrina Simader Jumanne 7 Februari 2017 Haki miliki ya picha AP
Image caption Siku iliyofuata, Mkenya Sabrina Simader anashuka kwa kasi kwenye mlima wakati wa mashindano ya ubingwa wa kuteleza kwenye barafu St Moritz, Uswizi.
Kibera, Nairobi, Kenya - Jumanne 7 Februari 2017 Haki miliki ya picha EPA
Image caption Na Jumanne pia, msichana huyu katika mtaa wa Kibera aliyeachwa akisimamia kibanda cha kuuzia viatu, anatazama mwenye kamera huku wanafunzi wakipita hapo karibu.

El-Riyadh camp in Geneina

Darfur Magharibi, Sudan - Jumatano 8 Februari 2017 Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wasichana wakiwa darasani katika kambi ya watu waliotoroka mapigano ya El-Riyadh mjini wa Geneina eneo la Darfur Jumatano nchini Sudan.
Vatican - Jumatano 8 Februari 2017 Haki miliki ya picha AFP
Image caption Siku hiyo pia, Papa Francis anainua picha ya mtakatifu Josephine Bakhita aliyetoka Sudan akiwa Vatican kwa misa ya kuadhimisha siku ya kumkumbuka. Bakhita alizaliwa Darfur na akatekwa na wafanyabiashara ya utumwa. Baadaye alikuwa mtawa Italia na kuhudumu kwa zaidi ya miaka 40.
Beji Caid EssebsiItalia Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Jumatano, walinzi wanampigia saluti Rais wa Tunisia Beji Caid Essebsi alipokutana na Waziri Mkuu wa Italia Paolo Gentiloni mjini Roma.
Tunis, Tunisia - Jumatatu 6 Februari 2017 Haki miliki ya picha EPA
Image caption Siku mbili awali, walinzi maalum wa rais wa Tunisia wanaonekana wakijiandaa kwa gwaride katika mji mkuu wa Tunis, kuadhimisha miaka minne tangu kuuawa kwa kiongozi wa upinzani Chokri Belaid.
Jacob Zuma 9 Februari 2017 Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma anaonekana kufahamu yanayomsubiri anapoelekea kutoa hotuba bungeni Alhamisi. Wabunge wa upinzani walijaribu kuvuruga hotuba yake.
Bunge Afrika Kusini 9 Februari 2017 Haki miliki ya picha EPA
Image caption Wanajeshi walitumwa kudumisha usalama… hapa, maafisa maalum wanaonekana wakishika doria kwenye paa za Majengo ya Bunge Cape Town...
Cape Town- 9 Februari 2017 Haki miliki ya picha EPA
Image caption Sherehe ya kufunguliwa kwa vikao vya Bunge huwa wakati wa kujipamba kwa wanaohudhuria...
Cape Town, 9 Februari 2017 Haki miliki ya picha AFP
Image caption Ndani ya bunge, vurugu zilizuka Zuma alipoanza kuhutubu...nje, polisi waliwatenganisha wafuasi wa serikali na upinzani.
Johannesburg, 9 Februari 2017 Haki miliki ya picha EPA
Image caption Hapa bado ni Afrika Kusini, lakini ni wakati wa mazoezi kwa mashindano ya mbio za ngalawa ya Dusi ambayo yataanza wiki ijayo.
Zanzibar, Tanzania - 9 Februari 2017 Haki miliki ya picha Sammy Awami/BBC
Image caption Na iwapo utakuwa Zanzibar wikendi hii, usikose tamasha la Sauti za Busara. Hapa, watumbuizaji wanaonekana Mji Mkongwe Alhamisi wakati wa matembezi ya kufungua rasmi tamasha hilo.

Images courtesy of AP, AFP, EPA, Reuters

Mada zinazohusiana