Malumbano kuhusu mazishi ya Tshisekedi yazuka DRC

Etienne Tshisekedi alifariki akiwa nchini Ubelgiji
Image caption Etienne Tshisekedi alifariki akiwa nchini Ubelgiji

Mipango ya kurudisha mwili ya kiongozi wa upinzani wa muda mrefu nchini DRC Etienne Tshisekedi hadi mjini Kinshasa kwa mazishi, imekumbwa na matatizo kuhusu mipango ya mazishi hayo.

Serikali ya Congo imeahidi kuruhusu juneza lake kupelekwa bungeni na pia kusema kuwa itawalipia ndege waliokuwa wanasiasa wenzani hadi mjini Brussels kuuchukua mwili huo.

Lakini chama chake Tshisekedi cha Union for Democracy and Social Progress (UDPS), kumekataa pendekezo hilo na badala yake kutangaza masharti yake.

Kinasema kuwa serikali inastahili kumjengea makumbusho bwana Tshisekedi kati kati ya mji wa Kinshasa na pia kimetaka gharama ya mazishi kulipwa na serikali inayokuja ambayo muundo wake umeafikiwa, lakini ambayo bado haijaingia madarakani.

Maafikiano ya kubuniwa serikali mpya inayojumuisha muungano wa upinzani uliobuniwa na bwana Tshisekedi, ilikuwa na sehemu ya ugavi wa mamlaka ulioafikiwa mwaka uliopita.

Serikali imejibu masharti ya UDPS ya kujengwa kwa makumbusho lakini imesema kuwa hayatajengwa kati kati mwa mji.

Image caption Chama chake Tshiskedi (UDPS), kumetangaza masharti yake.