Donald Trump asema atatoa marufuku mpya

Marufuku hiyo ya Trump ilizua ghasia katika viwanja vya ndege na kusababisha maandamano nhcini humo Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Marufuku hiyo ya Trump ilizua ghasia katika viwanja vya ndege na kusababisha maandamano nhcini humo

Donald Trump anasema kuwa huenda akabadilisha marufuku yake dhidi ya wahamiaji na agizo jingine la rais litakalopiga marufuku raia wa mataifa kadhaa kutoingia Marekani baada ya jaribio lake la awali kubadilishwa na mahakama.

Bw Trump aliambia wanahabari katika ndege ya Airfoce One kwamba amri mpya huenda ikatolewa mapema siku ya Jumatatu ama jumanne .

Inajiri baada ya mahakama ya rufaa mjini San Fransisco kupinga amri yake ya hapo awali.

Agizo hilo lilikuwa limepiga marufuku raia kutoka mataifa saba ya Waislamu.

Haijulikani ni vipi amri hiyo mpya itakuwa.

Bw Trump amesema kuwa amri hiyo itakuwa na mabadilik kidogo lakini hakutoa maelezo zaidi.

Image caption Serikali ya Marekani

Licha ya pendekezo lake siku ya Ijumaa ,serikali ya Trump huenda ikafuatilia rufaa yake mahakamani kuhusu agizo lake la kwanza ambalo lilipingwa wiki moja iliopita na jaji wa Seattle.

''Tutashinda vita hivi,Trump aliwaambia maripota akiongezea:Tatizo ni kwamaa inachukua muda mwingi.Lakini tutashinda vita hivyo.Lakini pia tuna njia nyengine mbadala ikiwemo kuanzisha upya marufuku nyengine''.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii