Moto mkubwa waitishia Australia

Moto New South Wales Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Moto New South Wales

Ilani imetolewa kuwa janga kubwa la moto linaweza kutokea katika jimbo la New South Wales la Australia kwa sababu ya joto jingi.

Mkuu wa idara ya wazima moto ya jimbo hilo, alisema hali hivi sasa ni mbaya sana.

Wazima moto zaidi ya elfu moja wanapambana na myoto kama 80 sehemu mbali mbali za jimbo, huku joto limefika kipimo cha nyuzi 45 Celsius.

Image caption New South Wales

Upepo mkali nao unachangia kusambaa kwa myoto hiyo.

Joto jingi piya limetatiza huduma za umeme.

Baadhi ya makarakana, pamoja na karakana kubwa kabisa ya Australia ya kusafisha aluminium, yamepunguza kazi au kufungwa kabisa ili kuhifadhi umeme.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Moto New South Wales
Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Moto New South Wales