Steinmeier achaguliwa Rais mpya wa Ujerumani

Bwana Steinmeier akiwasili bungeni na mkewe Elke Buedenbender Haki miliki ya picha EPA
Image caption Bwana Steinmeier akiwasili bungeni na mkewe Elke Buedenbender

Waziri wa zamani wa mashauri ya nchi za nje wa Ujerumani, Frank-Walter Steinmeier, amechaguliwa kuwa rais mpya ya Ujerumani, pale wabunge na waakilishi wa taifa walipopiga kura hii leo.

Bwana Steinmeier anaungwa mkono na vyama vikuu vya kisiasa.

Mwaka jana, alipokuwa waziri wa mashauri ya nchi za nje, alimuelezea Donald Trump kuwa mhubiri wa chuki.

Baada ya uchaguzi wa Marekani, alisema, anapata shida kutambua msimamo wa Bwana Trump kuhusu sera zake za mashauri ya nchi za nje.

Rais wa Ujerumani hana madaraka ya utendaji, lakini anafikiriwa kuwa kiongozi wa maadili ya nchi.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wabunge wa Ujerumani